Skip to main content

Posts

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY MIMBA ZABIBU: Ni uvimbe unaotokea baada ya mbegu ya kiume kurutubisha yai la kike kwenye mji wa mimba (uzazi). Uvimbe huu baada ya kutengenezwa huendelea kukua na kuongezeka ukubwa kama mimba ya kawaida. Baada ya muda flani huanza kuleta au kuonyesha dalili za mtu Mwenye mimba au mjamzito. Uvimbe huu umetengenezwa na Tishu au kuta za mji wa mimba au uzazi. Kwa kawaida hali hii au uvimbe huu unaweza ukawa saratani au usiwe saratani, awali huanza kawaida ila kwa baadae unaweza ukawa saratani (kansa). NAMNA INAVYOTOKEA | CHANZO | KISABABISHI. Kwa kawaida ili mimba itungwe lazima mbegu ya kiume ikutane na yai la kike, na pande zote mbili upande wa mbegu za kiume na wakike lazima kuwe na vinasaba. Kama yai la kike halina vinasaba hutengeneza mimba zabibu (molar pregnancy) inayojulikana kama partial molar pregnancy, uvimbe huu huendelea kuongezeka ukubwa kama fung...

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KIPINDI CHOTE CHA UJAUZITO

Mama mjamzito ni muhimu kuzingatia vitu vifatavyo ili kuepuka Madhara ya kiafya kwa Mama na mtoto. 1.Punguza matumizi ya vyakula vyenye “caffeine” Kama vile chai, kahawa na soda za cola huweza kusababisha mimba kuharibika au kutoka.  2.  Kula vizuri chakula chenye mlo kamili na aina mbalimbali za matunda ili kujenga afya yako na ya mtoto. 3. Pata muda wa kutosha wa kupumzika ili kutuliza mwili na akili kwa afya yako na ya mtoto. 4. Fanya mazoezi madogo madogo ya viungo kama kutembea, kuogelea na yoga mara kwa mara 5. Kunywa dawa za kuongeza vitamini mwilini “Pregnancy vitamin” endapo huna uwezo wa kula chakula chenye mlo kamili lakini isiwe mbadala wa chakula 6. Acha kuvuta sigara kama ni mtumiaji kwani husababisha madhara kwako na pia mimba kutoka, kuzaa mtoto kabla ya siku kutimia na mtoto kufariki akiwa tumboni. ∆ Acha kunywa pombe       Mjazito anapotumia pombe kwani humfikia mtoto kupitia mirija ya damu na kondo la nyama ( placenta) na ku...

KIFAHAMU KISUKARI KIPINDI CHA UJAUZITO | CHANZO/SABABU | DALILI ZAKE | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUKIEPUKA.

KIFAHAMU KISUKARI KIPINDI CHA UJAUZITO | CHANZO / SABABU | DALILI ZAKE | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUKIEPUKA . KISUKARI Ni moja ya  kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na  mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo VITU VINAVYOWEZA KUPELEKEA MTU KUPATA KISUKARI : ♦ Kuwahi kujifungua mtoto mwenye Uzito mkubwa 4000g (4kg) kwa mimba/Ujauzito uliopita. ♦ Kuwa na historia kwenye familia ya mtu mwenye kisukari/kuridhi. ♦ Kuwa unene au Uzito mkubwa kuliko kawaida. ♦ Kuwa na shinikizo la juu la damu (presha) ♦ Kuwa na Mafuta mengi | cholesterol ♦ Kuwa na kisukari aina ya kwanza au ya pili. AINA ZA KISUKARI : Kuna ainaTatu za kisukari KISUKARI AINA YA KWANZA | DIABETES TYPE 1     ♦ Ni aina ya kisukari ambacho mtu anazaliwa nacho/kuridhi kutoka ...

ALL BEAUTIFUL SCRUBS (SURGICAL GOWNS)  AND MEDICAL | LAB- COATS FOR MALE  AND FEMALE ARE AVAILABLE

GOOD NEWS TO YOU : ALL BEAUT IFUL SCRUBS (SURGICAL GOWNS)  AND LAB COATS FOR MALE  AND FEMALE ARE AVAILABLE TO US ,SO ITS YOUR TIME NOW TO CONTACT US FOR GOOD SERVICES 0THER EQUIPMENTS ARE LIKE STETHOSCOPE ♦ Littman class II ♦ Littman master class II ♦ Littman class III ♦ Dual head stethoscope ♦ Transparent Sprague Rappaport stethoscope ♦ MDF Stethoscope (Adult) ♦ MDF deluxe Infant and Neonate Stethoscope ♦ Stainless Steel stethoscope For Adult TAPE MEASURES of different in morden  types BP MACHINE ♦ Upper  arm automatic digital blood pressure monitor ♦ Wrist type automatic digital pressure monitor ♦ Upper arm automatic digital blood pressure monitor ♦ Aneroid sphygmomanometer -Palm Type Sphygmomanometer ♦ Palm Type Sphygmomanometer -Bokang Sphygmomanometer ♦ Splenger Blood pressure monitor -Riesta Blood pressure Monitor -Omrin Semi automatic blood pressure monitor REFLEX HUMMER ( PATELLA HUMMER) ♦ General reflex hummer  ♦ Fallow hummer...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...

NJIA YA MPANGO YA LUPU (KITANZI)

NJIA YA UZAZI WW MPANGO YA LUPU | KITANZI LUPU  ( VITANZI )  Ni moja ya njia ya uzazi wa mpango inayotumiwa na wanawake wengi kwa lengo la kuzuia kupata mimba au kupanga uzazi Kifaa  hiki kimetengenezwa kwa kutumia kopa kina kama vijitawi kwa mbele Kifaa hiki kimetengenezwa na kuwekewa homoni ya Aina ya progestin ambayo inafanana  sana na homoni aliyonayo mwanamke. LUPU kina mkinga mwanamke asipate mimba kwa miaka 12. JINSI GANI NJIA HII INAFANYA KAZI .. • Kina mkinga asipate mimba kwa muda wa miaka 12 kwa.  • Kutoruhusu mbegu za kiume kutofika kwenye mirija ya uzazi • Huzuia urutubishaji wa yai la kike  kama zikifanikiwa kuingia kwenye mji wa mimba • Huzuia mbegu kuingia kwenye mji wa mimba kwenda kurutubisha yai la kike FAIDA ZA NJIA HII .. • Inazui mimba zisizo na mpangilio  • Ni salama kwa mtumiaji • Haisumbui kutoa na kuweka kwa mtumiaji  • Haichukui muda mrefu kurudi kwenye Hali ya kawaida na k...

MADHARA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI.

Kufanya mapenzi/kushiriki tendo wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana. Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si mazuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi. Yafatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati mwanamke yupo katika siku zake {period}   MADHARA KWA MWANAUME . 1. Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.   2. Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.   3. Kuziba kwa njia ya mkojo.   4. Utasa au ugumba.   5. Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.   6. Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu ha...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...

VITU | MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZIZO

VITU | MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZIZO . SABABU ZINAZO SABABISHA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA | KUBEBA UJAUZITO | MIMBA Jinsia zote mbili zinaweza kuchangia Kushindwa kutunga kwa mimba Mwanamke anaweza akawa amewahi kuzaa / kubeba ujauzito awali au Hajawahi kubeba Ujauzito na ikawa shida kushika ujauzito kwa sababu kadha wa kadha ambazo zinaweza kutoka kwa mwanamke au mwanamme. MWANAMME ANAWEZA KUCHANGIA KIVIPI MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO • Matatizo yaTezi dume • Kutoa mbegu ambazo hazijakomaa • Kutoa Mbegu chini ya kiwango (idadi) • Upungufu wa nguvu za kiume • Tatizo la msongo wa mawazo,kukosa usingizi,Kusafiri kwa safari ndefu Mara kwa Mara • Kuzidisha Matumizi ya dawa • Upungufu wa damu kwa muda mrefu SABABU ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO . • Maambukizi kwenye via vya uzazi • Uvimbe kwenye kwenye mirija ya uzazi • Mirija ya uzazi Kujaa maji • Kuwa mvurugiko wa homoni • Umri zaidi ya miaka 35 • Kuw...

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KWA MWANAMKE

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI Ni moja ya sababu inayopelekea mwanamke Kushindwa kubeba /kushika mimba. - Mirija ya Uzazi ina weza kuziba kwa sababu mbali mbali. - Kuziba kwa mirija ya uzazi ni moja ya sababu kubwa ya Ugumba kwa wanawake. SABABU ZINAZOWEZA PELEKEA MWANAMKE KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI NI... - Kuwa na Uvimbe ambao umeota kwenye mirija ya uzaziz - Kuwa na Ugonjwa wa maambukizi ya kizazi na Nyonga. - Kuwa na historia ya mimba kutunga nje ya kizazi. - Magonjwa ya zinaa na upasuaji wa tumbo au uvimbe kwenye ukuta wa uzazi. - Kuwa na maambukizi kwenye mirija yaliyo sababishwa na utoaji wa mimba, kupasuka kwa kidole tumbo. - Uzazi wa mpango (Lupu/Kitanzi) - Ajari iliyo husisha Tumbo. - Mirija kujaa maji. DALILI ZA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI - Maumivu wakati wa kujamiana /Tendo - Maumivu makali ya nyonga na Tumbo kwa chini. - Kupata hedhi matone ikiambatana na Maumivu makali/Kupata damu nyingi Wakati wa hedhi. - Maumivu makali wakati wa ...

MAAMBUKIZI YA FANGASI KIPINDI CHA UJAUZITO | KIFAHAMU CHANZO | CHANZO | DALILI | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUJIKINGA.

MAAMBUKIZI YA FANGASI KIPINDI CHA UJAUZITO | KIFAHAMU CHANZO | CHANZO   | DALILI    | UCHUNGUZI   | MATIBABU | NAMNA YA KUJIKINGA . FANGASI Ni maambukizi yanayoweza Jittokeza sehemu yoyote ya mwili. Kuna aina kadha wa kadha ya fangasi na majina hutegemea na sehemu ya mwili walipo. FANGASI WA UKENI - KIPINDI CHA UJAUZITO Hawa ni moja ya fangasi ambao husumbua na hujitokeza kwa Wajawazito au kipindi cha Ujauzito na hushambulia sehemu ya uke. Fangasi ambao hushambulia kipindi cha ujauzito wanajulikana kwa jina la candida albicans Kipindi cha Ujauzito kuna mabdiliko ya Homoni ambazo kupelekea kubadilika kwa uasidi na ualikali (PH) ya Uke, na kuruhusu fangasi kuota kirahisi. Kipindi cha ujauzito homoni aina ya estrojeni(estrogen) inakuwa nyingi kuliko zingine na kufanya mazingira rafiki kwa fangasi kuota. Kuna sababu kadha wa kadha ambazo zinapelekea mjamzito kupata fangasi Mara kwa Mara . CHANZO | SABABU • Matumizi ya Dawa aina ya ...

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO AKIWA TUMBONI

Je wewe ni mjamzito na unatamani kufahama Hatua ya ukuaji wa mtoto wako aliyeko tumboni ?? Hizi ndio Hatua za ukuaji wa mwanao akiwa tumboni. Hatua za ukuaji wa mtoto tumboni WIKI YA (1- 4). √  Yai la kike linarutubishwa na mbegu za kiume. √  Kijusi kinaanza kujitengeza (Umba) √  Mishipa ya damu,Tumbo,Ini, n.k vinatengenzwa WIKI YA (5 - 8). Viungo Muhimu vinatengenzwa na kukomaa √  Ubongo √  Moyo √  Uti wa Mgongo √  Macho,masikio,mdomo na pua. √  Miguu, mikono, vidole na kucha WIKI YA (9-12). √  Shingo huanza kujitengenza. √  Kope za macho hujitengeneza. √  Katika kipindi hiki mtoto anafikia urefu wa inchi 2.5 Kumb .... Uhitaji mwingi wa madini ya chuma kwa mtoto. WIKI YA (13-17). √  Miguu na mikono inakamilika √  Shingo inakamilika katika kipindi hiki. √  Mifupa inaanza kukomaa WIKI YA (18-22). √  Mtoto anaweza  Kusikia sauti za mama yake. √  Mtoto anaanza kucheza tumboni. ...

LISHE WAKATI WA UJAUZITO NA WAKATI WA KUNYONYESHA

LISHE WAKATI WA UJAUZITO NA WAKATI WA KUNYONYESHA. Kipindi chote cha Ujauzito na wakati wa kunyonyesha Mama anahitajika kupata chakula cha kutosha kwa ajili ya Kiumbe kilicho tumboni pamoja na mama mwenyewe. Mama anaye nyonyesha anahitaji mlo ulio sahihi kwa ajili ya kusaidia kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto na kukupa nguvu na virutubisho vyote muhimu mwilini. FAIDA ZA LISHE BORA • Husaidia kuongeza damu na kuzuia upungufu wa damu • Husaidia kuongeza uzito kulingana na umri wa mama na mtoto na kuzuia kupata Utapiamlo. • Huimalisha ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili. • Husaidia kuzuia kupata mtoto mwenye uzito pungufu. • Humsaidia mama kuandaa  mwili na utengenezaji  wa maziwa ya kutosha wakati wa kunyonyesha. MAMBO YA KUZINGATIA. • Kabla ya kuweka chochote kinywani na baada ya kutumia choo nawa  mikono yako kwa maji safi na Salama na sabuni. • Anza kuhudhuria kliniki mapema baada ya kuhisi  ni mjamzito na mpeleke mtoto kliniki mapema kwa ajili y...