Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto
1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe
2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen.
kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen
• Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A
• Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B
• Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB
• Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O
3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor
3.(a) Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya +
mfano A+, B+, AB+ au O+
3. (b) Mtu ambaye cell zake nyekundu hazina hii antigen D, blood group yake inaandikwa na alama -
mfano A-, B-, AB- au O-
4. hii alama ya + au - inapatikana je?
4. (a) Baba hutoa Rh moja kwa mtoto, inaweza kuwa Rh+ au Rh- na mama hutoa Rh moja inaweza kuwa Rh+ au Rh-
4. (b) mtoto akizaliwa akiwa na Rh - manake baba alitoa Rh- na mama alitoa Rh -
4. (c) Mtoto akiwa Rh+ anaweza kuwa baba alitoa Rh+ na mama alitoa Rh+
mtoto mwenye Rh + anaweza kuwa alipata Rh- na Rh + ila hatuoandika Rh+Rh- kwa sababu Rh- ni kma haipo
UCHUMBA NA KUZAA /UJAUZITO
• Mvulana akiwa na damu yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ )
• Anaweza kuoana na msichana yeyote mwenye damu group yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ ) na watapata watoto bila tatizo lolote.
• Mvulana akiwa na group mfano ( A+, B+, AB+ au O+) akioa msichana mwenye A-, B-, AB- au O-
6. (a) Mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri, na ikitokea MSICHANA AMEJIFUNGULIA NYUMBANI au NJE YA HOSPITAL, ambako hakugundulika kwamba ana damu negative... Mtoto wa kwanza ataishi vizuri kabisa na afya nzuri. ila watoto wanaofata hawataweza kuishi au watakufa kabla hawajazaliwa kwa sababu,
6. (b) Msichana mwenye negative blood group ( Rh-) yaani hana D antigen, alipojifungua mtoto wa kwanza mwili wake unakuwa sasa umeandaa kujikinga (antibodies kupambana na D antigen ( Rh +) kwa baadae
• MTOTO WA PILI akitungwa mwili wa mama tayari una Antibodies dhidi ya Rh+ ( mtoto anazo hizi Rh+), hivyo matokeo yake ni kuwa seli nyekundu za mtoto zitashambuliwa na kufa.
• Mtoto akibahatika kuzaliwa hai, atapoteza uhai muda sio mrefu kwa vile anakuwa hana seli nyekundu za kusambaza damu mwilini.
7. Endapo Msichana huyu alijifungulia MTOTO WA KWANZA HOSPITAL, madaktari wanakuwa wameshajua kwamba ana damu negative, hivyo wanasaidiana na mmewe kufanya maandalizi ya sindano yenye dawa ( SIITAJI HAPA )
alafu msichana akijifungua tuu MTOTO WA KWANZA anachomwa hiyo sindano na akija kupata mimba baada atachomwa hiyo sindano wakati wa mimba na pindi anapojifungua.
Hii kitu imenielimisha Sana jamani watanzania tupende kusoma na kuperuzi vitu elimu Kama hii imewekwa wazi lakini bado hatuijui.
ReplyDeleteKwamfano baba group o +negative na mama group o +negative mtoto atakuwa group gan la dam
DeleteBinafsi nashukuru sana kwa elimu hii ni nzuri sanaaaa
ReplyDeleteUko sawa
DeleteNashkuru sana kwa Elimu hii nzuri nimefurahi sana kujuwa hili. Nakumbuka kijijini kwetu kuna Familia walizaa mtoto wa kwanza akaishi waliofatia wote walikuwa wakizaliwa na kufa. kutokana na ile familia hawakuwa na Elimu walisema kuwa upande wa mwanamke huko kwao ni wachawi hivyo ilipelekea ile ndoa kuvunjika. Yule mwanaume alikuja kuoa mwanamke mwingine na alizaa naye watoto wanne wote wapo hai. Wangekuwa na elimu wangelielewa hili Elimu ni Ufunguo Barikiwa sana kwa kutuelemisha.
ReplyDeleteHello Habari Naomba kuuliz Mimi mwanaume Nina blood group A-negative na mke wangu and blood group O+positive kuna shiida us uzazi? Maana kila Akibeba mimba zinaharibika
ReplyDeleteKwa uelewa wangu hapo group hilo halina shida
DeleteHamna tatizo hapo ndugu
DeleteMimi nina o- na mke wangu ana o+ vip hapo kunashida yeyote?
DeleteElimu hii ni nzuri sana, iwapo watu wangelikuwa wanafatilia mada kama hizi basi wangeweza kuepusha madhara mengi yanayojitokeza kwenye uzazi.
ReplyDeleteHabari mimi Nina group 0+ na bwana B- inakuwaje hapoo
ReplyDeleteHapo hamna shida, Shida ingekuwepo kama wewe unge kuwa na (-) na mtoto wa Kwanza angekuja akazaliwa ni (+)
DeleteHabari!samahani Mimi kundi langu la damu ni AB+ na mume wangu ni 0- vp hapa Dr.?naomba msaada.
DeleteNashukuru kwa elimu na u
ReplyDeleteshauri mzuri
Mi nauliza ofisi zenu zipo wapi nahitaji argi + bei gani
ReplyDeleteJamn me mwanamke group lang la damu O+ na mume wangAB+ kuna uhakika wa kubeba mimba maana nilibeba ya kwanza ikatoka ikiwa na wiki 6
ReplyDeleteHapa nimepata Elimu juu ya hivi vitu adhimu, kwamba kabla ya kuanzisha mahusiano ni vema kuchunguzana juu ya hizi blood groups. Hata hivyo nimeelewa Kitu cha msingi kwamba msichana mwenye Rh+ anaolewa na yeyote yaani mvulana mwenye Rh+ au Rh- na anapata watoto bila tatizo kabisa. Ila msichana mwenye Rh- anatakiwa kuolewa na mvulana mwenye Rh- hapo atazaa watoto wote bila tatizo. Na mvulana akiwa na Rh+ akaoa msichana mwenye Rh- mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri na kukua vema ila watoto watakaofuata watapata matatizo ikiwa tatizo halitagundulika kwa uzazi wa kwanza akachomwa sindano. Nimeelewa somo hadi natamani kuelimisha wengine vijijini huko ni shida.
ReplyDelete