Skip to main content

Posts

Showing posts with the label AFYA YA UZAZI

Tatizo la Kutokwa na uteute /Uchafu au majimaji kwenye uke

VAGINAL DISCHARGE. (Kutokwa na uteute /Uchafu au majimaji kwenye uke) Miongoni mwa masomo ambayo tulijifunza huko nyuma ni juu ya umuhimu wa kutokwa na uteute au majimaji kwenye uke,somo liliwafungua wengi maana wengi walikuwa wakiona wanatokwa na ute bila kujua kazi yake au unaashiria nini. Mmbali na umuhimu wa uteute au majimaji yanayotoka kwenye uke, kumekuwa na maswali mengi na yanayoongozana kuhusu aina ya uteute unatoka kwenye uke, jambo ambalo limeonesha kuwapa hofu wengi juu ya afya zao pindi wauonapo ute ukiwatoka je kutokwa na uteute ni kawaida? Ndio,Tezi ndani ya uke wako na njia ya uzazi huzalisha kiasi kidogo cha majimaji ambacho hutuka kupitia uke kila siku, huku kikiwa kimebeba seli za zamani ambazo hazina kazi mwilini na kuzitoa kama uchafu, Hiyo ni njia ya kuufanya uke wake kuwa msafi na kulinda afya yake, ute huo unatoka huwa ni msafi wenye kuonekana vizuri au mfanano wa maziwa maziwa na hautoi harufu mbaya. (Uke kwa kawaida hautakiwi kuwa mkamvu, na tulishajifun...

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY MIMBA ZABIBU: Ni uvimbe unaotokea baada ya mbegu ya kiume kurutubisha yai la kike kwenye mji wa mimba (uzazi). Uvimbe huu baada ya kutengenezwa huendelea kukua na kuongezeka ukubwa kama mimba ya kawaida. Baada ya muda flani huanza kuleta au kuonyesha dalili za mtu Mwenye mimba au mjamzito. Uvimbe huu umetengenezwa na Tishu au kuta za mji wa mimba au uzazi. Kwa kawaida hali hii au uvimbe huu unaweza ukawa saratani au usiwe saratani, awali huanza kawaida ila kwa baadae unaweza ukawa saratani (kansa). NAMNA INAVYOTOKEA | CHANZO | KISABABISHI. Kwa kawaida ili mimba itungwe lazima mbegu ya kiume ikutane na yai la kike, na pande zote mbili upande wa mbegu za kiume na wakike lazima kuwe na vinasaba. Kama yai la kike halina vinasaba hutengeneza mimba zabibu (molar pregnancy) inayojulikana kama partial molar pregnancy, uvimbe huu huendelea kuongezeka ukubwa kama fung...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...

MADHARA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI.

Kufanya mapenzi/kushiriki tendo wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana. Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si mazuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi. Yafatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati mwanamke yupo katika siku zake {period}   MADHARA KWA MWANAUME . 1. Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.   2. Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.   3. Kuziba kwa njia ya mkojo.   4. Utasa au ugumba.   5. Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.   6. Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu ha...

VITU | MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZIZO

VITU | MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZIZO . SABABU ZINAZO SABABISHA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA | KUBEBA UJAUZITO | MIMBA Jinsia zote mbili zinaweza kuchangia Kushindwa kutunga kwa mimba Mwanamke anaweza akawa amewahi kuzaa / kubeba ujauzito awali au Hajawahi kubeba Ujauzito na ikawa shida kushika ujauzito kwa sababu kadha wa kadha ambazo zinaweza kutoka kwa mwanamke au mwanamme. MWANAMME ANAWEZA KUCHANGIA KIVIPI MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO • Matatizo yaTezi dume • Kutoa mbegu ambazo hazijakomaa • Kutoa Mbegu chini ya kiwango (idadi) • Upungufu wa nguvu za kiume • Tatizo la msongo wa mawazo,kukosa usingizi,Kusafiri kwa safari ndefu Mara kwa Mara • Kuzidisha Matumizi ya dawa • Upungufu wa damu kwa muda mrefu SABABU ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO . • Maambukizi kwenye via vya uzazi • Uvimbe kwenye kwenye mirija ya uzazi • Mirija ya uzazi Kujaa maji • Kuwa mvurugiko wa homoni • Umri zaidi ya miaka 35 • Kuw...

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KWA MWANAMKE

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI Ni moja ya sababu inayopelekea mwanamke Kushindwa kubeba /kushika mimba. - Mirija ya Uzazi ina weza kuziba kwa sababu mbali mbali. - Kuziba kwa mirija ya uzazi ni moja ya sababu kubwa ya Ugumba kwa wanawake. SABABU ZINAZOWEZA PELEKEA MWANAMKE KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI NI... - Kuwa na Uvimbe ambao umeota kwenye mirija ya uzaziz - Kuwa na Ugonjwa wa maambukizi ya kizazi na Nyonga. - Kuwa na historia ya mimba kutunga nje ya kizazi. - Magonjwa ya zinaa na upasuaji wa tumbo au uvimbe kwenye ukuta wa uzazi. - Kuwa na maambukizi kwenye mirija yaliyo sababishwa na utoaji wa mimba, kupasuka kwa kidole tumbo. - Uzazi wa mpango (Lupu/Kitanzi) - Ajari iliyo husisha Tumbo. - Mirija kujaa maji. DALILI ZA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI - Maumivu wakati wa kujamiana /Tendo - Maumivu makali ya nyonga na Tumbo kwa chini. - Kupata hedhi matone ikiambatana na Maumivu makali/Kupata damu nyingi Wakati wa hedhi. - Maumivu makali wakati wa ...