VAGINAL DISCHARGE.
(Kutokwa na uteute /Uchafu au majimaji kwenye uke)
Miongoni mwa masomo ambayo tulijifunza huko nyuma ni juu ya umuhimu wa kutokwa na uteute au majimaji kwenye uke,somo liliwafungua wengi maana wengi walikuwa wakiona wanatokwa na ute bila kujua kazi yake au unaashiria nini.
Mmbali na umuhimu wa uteute au majimaji yanayotoka kwenye uke, kumekuwa na maswali mengi na yanayoongozana kuhusu aina ya uteute unatoka kwenye uke, jambo ambalo limeonesha kuwapa hofu wengi juu ya afya zao pindi wauonapo ute ukiwatoka je kutokwa na uteute ni kawaida?
Ndio,Tezi ndani ya uke wako na njia ya uzazi huzalisha kiasi kidogo cha majimaji ambacho hutuka kupitia uke kila siku, huku kikiwa kimebeba seli za zamani ambazo hazina kazi mwilini na kuzitoa kama uchafu,
Hiyo ni njia ya kuufanya uke wake kuwa msafi na kulinda afya yake, ute huo unatoka huwa ni msafi wenye kuonekana vizuri au mfanano wa maziwa maziwa na hautoi harufu mbaya. (Uke kwa kawaida hautakiwi kuwa mkamvu, na tulishajifunza kwanini ute unakuwa mkavu na jinsi gani ya kuufanya uweze kuwa na majimaji)
Rangi na uzito wake hubadilika kila siku katika mzunguko wa mwezi, ute huo unakuwa mzito endapo utakuwa katika kipindi cha kuangua mayai, kunyonyesha au umepandwa na hisia za kufanya mapenzi (nyege).
DALILI
Dalili gani zitakuonesha kwamba ute unaotoka si wa kawaida na kuashiria tatizo?
Dalili ambazo zitakuashiria ute unaotoka si wa kawaida ni,
-Kiasi cha utokaje wake (kingi)
-Harufu yake (mbaya)
-Rangi yake ( inakuwa tofauti na ute wa kawaida ambao ni mwepesi, unaonekana vizuri au wenye mfanano na maziwa maziwa)
-Uke unachoma choma au kama unawaka moto.
-Ute kutoka ukiwa umechanganyika na damu, ukiwa haupo kwenye kipindi chako cha hedhi.
Hii inaitwa vaginatis.Vaginitis ni hali ya uke kuvimba ambayo hupelekea kutoa majimaji au uteute usiokuwa wa kawaida. utakapoona dalili hizi juu mapema wahi hospitali kwaajili ya tiba,
Kutokwa na uteute au majimaji yasiyokuwa ya kawaida kwenye uke pia huchangiwa na maambukizi au matatizo ya aina tatu,
-Yeast infections,
-Bacterial vaginosis
-Trichomoniasis
YEAST INFECTION.
YEAST- ni selli moja ya fangasi ambayo hujizalisha yenyewe na kujigawagawa ambayo hupelekea maambukizi ya ngozi na sehemu zote zenye unyevu unyevu (kama kwenye uke)
Kiasi kidogo cha fangasi hawa kwa kawaida hupatikana kwenye uke wa mwanamke lakini huwa hawana madhara, lakini endapo watakuwa zaidi na kuwa wengi husababisha hayo maambukizi, maambukizi haya sio kawaida kuyapata kwa mwenza wako wakati wa ngono.
Ni rahisi kuyapata maambukizi haya kama ni
-mtumiaji wa dawa za antibayotinks( za kuua bakteria)
-Mjamzito
-Una kisukari
-Kukaa na joto au jasho kwa muda mrefu ( nafikiri hii husababisha kundi kubwa kupata zaidi maambukizi haya kutokana na majukumu ya kila siku, ni vyeta kupata muda wa kuoga kuupoza mwili na kutoa jasho)
Wakati mwingine mwanamke anaweza kupata maambukizi haya pasipokuwa na sababu.
DALILI ZA MAAMBUKIZI HAYA.
-Utete unakuwa mweupe kama vile cottage cheese.
-Kuvimba na kuhisi maumivu kuzunguka uke.
-Kuhisi kunachoma choma
-Maumivu wakati wa kufanya ngono.
BACTERIAL VAGINOSIS
Ni maambukizi ya uke yanayo sababishwa na bakteria. Kwa kawaida, kuna bakteria "Wazuri" na baadhi ya "bakteria" wabaya katika uke.
Aina wazuri husaidia kudhibiti ukuaji wa aina wabaya.
Ugonjwa huu ni tatizo ambalo linaweza kuondoka lanyewe katika siku chache. Lakini inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi. Hivyo ni wazo nzuri kwenda hospital kupata matibabu.
DALILI ZAKE
-Majimaji au uteute unaotoka unakuwa mweupe, kijivukijivu au kama wanjano njano.
-Harufu yake inakuwa kama shombo la samaki, na inaongezeka baada ya kufanya mapenzi au ukiwa unaosha na sabuni,
-Uke kuvimba na kuwa na wekundu kwa mbali.
-kusikia maumivu wakati wakukojoa,
TRICHOMONIASIS
Trichomoniasis ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na protozoa parasite anayeitwa Trichomonas vaginalis unaweza kupata maambukizi ya ugonjwa huu lakini suoneshe dalili kwa muda mrefu, mara nyingi hupatikana kwa kufanya mapenzi bila kondomu.
DALILI ZAKE.
-Kutokwa maji, au uteute wenye rangi ya njano au kijivu.
-Kutoa harufu mbaya kwenye uke.
-Maumivu wakati unakojoa,
Mgonjwa mengine ya zinaa pia huchangia kutokwa na majimaji au uteute mchafu,
SABABU ZINAZOSABABISHA KUTOKWA NA MAJI AU UTEUTE MCHAFU,
Nini husababisha au kubadilisha uteute au majimaji ya kawaida kutoka kwenye uke kuwa sio kawaida?
Kama tulivyoeleza awali uke wa mwanamke una bakteria ambao ni wazuri na ambao si wazuri, kiwango cha bacteria kikizidi au wakitibuliwa kwenye uke husababisha uke kutoa harafu na kutoa uteute au majimaji machafu,
Vitu ambavyo vinaweza kupelekea au kusababisha kuwatibu bacteria hao na kuleta madhara ni kama,
-Matumizi ya kemikali kwenye uke, kuosha kwa kutumia shampuu ndani na nje ya uke.
-Kutumia sabuni zenye kemikali (medicted soap)
--Matumizi ya dawa zakuua bacteria
-Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
-Kuwa mjamzito.
-Kuwa na kisukari
Au maambukizi ya aina yoyote kwenye uke.
KUMBUKA
-kuosha uke kwa kutumia vitu vyenye kemikali sio kuufanya kuwa msafi bali ni kujiongezea matatizo ambayo kemikali itasababisha maambuki kwenye via vya uzazi na utashindwa kupata watoto.
UNAWEZAJE KUZUIA AU KUJILINDA KUTOKANA NA MAAMBUKIZI HAYA?
Jisafishe kila unapotoka chooni hata kama ni kukojoa (anza kusafisha mbele kwenye uke kisha umalizie nyuma, kuzuia kutoa vijidudu nyuma kupeleka mbele)
Usivae nguzo za ndani kwa muda mrefu na penda kuvaa nguo zenye matirial ya pamba.
Usitumie vitu vyenye kemikali kujisafisha kwenye uke,
Kama mafuta ya kondomu yanakudhuru, jiepushe nayo
- Usitumie pafumu kwenye uke,
- Toilet paper
- Hakikisha unatumia pedi zenye ubora.
Karibu.
Facebook - Well
Instagram - Well clinic
WhatsApp. - Well (0684127127-(0743)SMS.
Comments
Post a Comment