Skip to main content

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY


ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY

MIMBA ZABIBU: Ni uvimbe unaotokea baada ya mbegu ya kiume kurutubisha yai la kike kwenye mji wa mimba (uzazi).

Uvimbe huu baada ya kutengenezwa huendelea kukua na kuongezeka ukubwa kama mimba ya kawaida.

Baada ya muda flani huanza kuleta au kuonyesha dalili za mtu Mwenye mimba au mjamzito.

Uvimbe huu umetengenezwa na Tishu au kuta za mji wa mimba au uzazi.

Kwa kawaida hali hii au uvimbe huu unaweza ukawa saratani au usiwe saratani, awali huanza kawaida ila kwa baadae unaweza ukawa saratani (kansa).

NAMNA INAVYOTOKEA | CHANZO | KISABABISHI.
Kwa kawaida ili mimba itungwe lazima mbegu ya kiume ikutane na yai la kike, na pande zote mbili upande wa mbegu za kiume na wakike lazima kuwe na vinasaba.

Kama yai la kike halina vinasaba hutengeneza mimba zabibu (molar pregnancy) inayojulikana kama partial molar pregnancy, uvimbe huu huendelea kuongezeka ukubwa kama fungu la zabibu zilivyo na dalili huendelea kujitokeza kadri siku zinavyoz zidi ongezeka.

Lakini yai lenye vinasaba hurutubishwa na mbegu (gameti) za kiume mbili na kutengeneza kitu kinaitwa kiini tete. Baada ya muda kutatengenezwa kondo la nyuma ambalo litabadilika na kuwa tishu (uvimbe) na baadae kiini tete kuhabika kuwa  tishu na kufanya kuwa uvimbe wa tishu za mimba zabibu (molar) kamili.
Baada ya tishu za mimba zabibu kutengenezwa ndipo mtu anaanza kuona dalili mbaya za ujauzito wake.

KUNDI LA WATU AMBAO WAKO KWENYE HATARI YA PATA MIMBA ZABIBU NI WALE WENYE SIFA ZIFATAZO.

Umri mkubwa wa mama, baadhi ya tafiti huonyesha umri mkubwa zaidi ya miaka 40.

• Mama mwenye historia ya kupata mimba zabibu katika mimba zake zilizopita.

• Baadhi ya tafiti huonyesha upungufu wa virutubisho kama folic acid na vitamini A(carotene) kwa mama huongeza hatari ya kupata hali hii.

• Tafiti zingine huonyesha vitu kama uvutaji sigara kuongeza hatari ya hali hii.

KUMBUKA
         "Si kila mwanamke mwenyesifa tajwa hapo juu anapata mimba zabibu"

DALILI  | ISHARA ZA MIMBA ZABIBU

Dalili za  Tatizo zinafanana na kabisa na Dalili za mtu, Mwenye ujauzito wa kawaida kwa miezi mitatu ya mwanzo na mabadiliko huanza kuonekana kuanzia miezi 4 na kuendeleea.

Zifatazo ni baadhi ya dalili zinazoonekana kwa mtu Mwenye molar pregnancy.

• Kichefuchedu na kutapika isivyo kawaida zaidi ya hali ya kawaida ya kutapika akiwa mjamzito
• Kutokwa damu ukeni, hii huweza kuwa matone tu au damu nyingi.
• Mama kuona akitoka vitu venye mfano wa zabibu au vinyama kutoka ukeni
•  Maumivu ya tumbo
• Baadhi ya wanawake huweza kupata dalili zinazotokana na kuzidi kwa homoni iitwayo thyroid. Dalili hizi ni kama wasiwasi uliopitiliza, mapigo ya moyo kwenda mbio, kuhisi joto kupita kiasi, uchovu uliokithiri.
• Mama pia huweza kugundulika kuwa na presha kubwa (mgandamizo mkubwa wa damu) na hali hii hujitokeza mapema sana katika ujauzito. Wengine kupata dalili hii katika wiki 13 za mwanzo.
• Kutokusika kwa mapigo ya moyo ya mtoto, hali ambayo mama atapewa taarifa kliniki au mama mwenyewe kushindwa kusikia mtoto akicheza tumboni. Kawaida mtoto huanza kucheza tumboni kuanzia mimba yenye umri wa wiki 16-25.

UCHUNGUZI | VIPIMO

• Kipimo cha mimba
• Kupima kiwango cha homoni ya hCG
• Kupiga picha ya tumbo (Ultrasound scan)
• Kuchukua kinyama cha mimba zabibu na kukifanyia uchunguzi

MATIBABU | TIBA

• Pale inapobainika kuwa ni mimba zabibu hutibika  Kusafishwa kizazi kutoa mimba zabibu. (Suction & curettage)
Tiba ninyingine hutibika kwa kuondoa kizazi kama mimba zabibu imekuwa ikijirudia rudia kwa mtu husika.
Mgonjwa atapewa Dawa ya Kupunguza kiasi cha homoni ya hCG kama iko juu mpaka itakapo shuka.
•  Baada ya homoni ya hCG kushuka utashuriwa kuendelea kupima kama vifatavyo.

Utapima kila wiki kwa muda wa wiki 3 na baadae utaendelea kupima kila mwezi kwa muda wa miezi 6 huku ukiendelea kuchunguza kila mwezi na baadae kila miezi 3.
•Atapatiwa Dawa za kuzuia damu isitoke kwa wingi.
Atapatiwa Dawa za kuua bakteria na Kupunguza maumivu.
Matibabu mengine atafanyiwa kulingana na hali yake.

NAMNA YA KUZUIA / KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA MOLAR PREGNANCY.
Matumizi ya vitu vifatavyo husaidia Kupunguza uwezekano wa kupata Mimba zabibu (molar pregnancy)

•  Vyakula vyenye virutubisho vya ain ya protini
                  Kama vile - Samaki
                                     - Maharagwe
                                               
                                                                                • Matunda/Mboga mboga zenye kiasi cha madini  ya folic acid
  Epuka uvutaji wa sigara

NOTE:
          -Unashauriwa kukaa walau mwaka moja kabla ya kushika au kubeba ujauzito mwingine baada ya matibabu.
         - Pia mara  chache hutokea japo sio Mara nyingi kwamba mimba zabibu hujirudia kwenye ujauzito unaofata.

Comments

Popular posts from this blog

IFAHAMU ARGI PLUS (+) MAANA YAKE | KAZI ZAKE | FAIDA ZAKE | MATUMIZI YAKE

IFAHAMU ARGI PLUS (+) MAANA YAKE | KAZI ZAKE | FAIDA ZAKE | MATUMIZI YAKE FOREVER Argi+ ni bidhaa bora kabisa kutoka katika kampuni yetu ya Forever living products Ina L-arginine amino acid kwa kila kijiko kimoja cha Argi+ Ina Nitric oxide ambayo inasaidia kutanua mishipa ya damu hivyo kuruhusu damu kupita vizuri Ina viondosha sumu vya *POMOGRANATE* ambavyo ni muhimu sana ili kuondoa sumu mwilini Ina *Vitamin* *Complex* ambazo zinasaidia kujenga misuli FAIDA ZA KUTUMIA ARGI+ 1. Ni kirutubisho muhimu sana kutumiwa kila siku kwa ajiili ya kusaidia mifumo yote ya mwili ili kuupa mwili uwezo wa kufanya kazi vizui zaidi. 2. Inasaidia mfumo wa kinga ya mwili, kutokana na nitric oxide ambayo inatumiwa na chembechembe nyeupe za damu kuua bacteria. Hivyo kuupa mwili uwezo zaidi wa kupigana na magonjwa. 3. Inasaidia kurekebisha kiwango cha "blood pressure kiwe sahihi na afya ya mzunguko wa damu ya moyo kiujumla. 4. Inasaidia kutengenezwa kwa mifupa na mwili kiujumla hivyo ...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...