Skip to main content

Posts

Showing posts with the label UJAUZITO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto. ATHARI ZITOKANAZO NA MAMA MJAMZITO KULALIA MGONGO | CHALI | TUMBO. ∆ Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama, ∆ Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono) ∆ Kushuka au kupanda kwa blood pressure ∆ Ini kuelemewa uzito ∆ Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto ∆ Kusikia kizunguzungu mara kwa mara ∆ Kama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku ∆ Kukoroma ∆ Maumivu ya mgongo ∆ Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen) ∆ Mtoto kukosa virutubi...

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KIPINDI CHOTE CHA UJAUZITO

Mama mjamzito ni muhimu kuzingatia vitu vifatavyo ili kuepuka Madhara ya kiafya kwa Mama na mtoto. 1.Punguza matumizi ya vyakula vyenye “caffeine” Kama vile chai, kahawa na soda za cola huweza kusababisha mimba kuharibika au kutoka.  2.  Kula vizuri chakula chenye mlo kamili na aina mbalimbali za matunda ili kujenga afya yako na ya mtoto. 3. Pata muda wa kutosha wa kupumzika ili kutuliza mwili na akili kwa afya yako na ya mtoto. 4. Fanya mazoezi madogo madogo ya viungo kama kutembea, kuogelea na yoga mara kwa mara 5. Kunywa dawa za kuongeza vitamini mwilini “Pregnancy vitamin” endapo huna uwezo wa kula chakula chenye mlo kamili lakini isiwe mbadala wa chakula 6. Acha kuvuta sigara kama ni mtumiaji kwani husababisha madhara kwako na pia mimba kutoka, kuzaa mtoto kabla ya siku kutimia na mtoto kufariki akiwa tumboni. ∆ Acha kunywa pombe       Mjazito anapotumia pombe kwani humfikia mtoto kupitia mirija ya damu na kondo la nyama ( placenta) na ku...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...

MAAMBUKIZI YA FANGASI KIPINDI CHA UJAUZITO | KIFAHAMU CHANZO | CHANZO | DALILI | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUJIKINGA.

MAAMBUKIZI YA FANGASI KIPINDI CHA UJAUZITO | KIFAHAMU CHANZO | CHANZO   | DALILI    | UCHUNGUZI   | MATIBABU | NAMNA YA KUJIKINGA . FANGASI Ni maambukizi yanayoweza Jittokeza sehemu yoyote ya mwili. Kuna aina kadha wa kadha ya fangasi na majina hutegemea na sehemu ya mwili walipo. FANGASI WA UKENI - KIPINDI CHA UJAUZITO Hawa ni moja ya fangasi ambao husumbua na hujitokeza kwa Wajawazito au kipindi cha Ujauzito na hushambulia sehemu ya uke. Fangasi ambao hushambulia kipindi cha ujauzito wanajulikana kwa jina la candida albicans Kipindi cha Ujauzito kuna mabdiliko ya Homoni ambazo kupelekea kubadilika kwa uasidi na ualikali (PH) ya Uke, na kuruhusu fangasi kuota kirahisi. Kipindi cha ujauzito homoni aina ya estrojeni(estrogen) inakuwa nyingi kuliko zingine na kufanya mazingira rafiki kwa fangasi kuota. Kuna sababu kadha wa kadha ambazo zinapelekea mjamzito kupata fangasi Mara kwa Mara . CHANZO | SABABU • Matumizi ya Dawa aina ya ...

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO AKIWA TUMBONI

Je wewe ni mjamzito na unatamani kufahama Hatua ya ukuaji wa mtoto wako aliyeko tumboni ?? Hizi ndio Hatua za ukuaji wa mwanao akiwa tumboni. Hatua za ukuaji wa mtoto tumboni WIKI YA (1- 4). √  Yai la kike linarutubishwa na mbegu za kiume. √  Kijusi kinaanza kujitengeza (Umba) √  Mishipa ya damu,Tumbo,Ini, n.k vinatengenzwa WIKI YA (5 - 8). Viungo Muhimu vinatengenzwa na kukomaa √  Ubongo √  Moyo √  Uti wa Mgongo √  Macho,masikio,mdomo na pua. √  Miguu, mikono, vidole na kucha WIKI YA (9-12). √  Shingo huanza kujitengenza. √  Kope za macho hujitengeneza. √  Katika kipindi hiki mtoto anafikia urefu wa inchi 2.5 Kumb .... Uhitaji mwingi wa madini ya chuma kwa mtoto. WIKI YA (13-17). √  Miguu na mikono inakamilika √  Shingo inakamilika katika kipindi hiki. √  Mifupa inaanza kukomaa WIKI YA (18-22). √  Mtoto anaweza  Kusikia sauti za mama yake. √  Mtoto anaanza kucheza tumboni. ...