Skip to main content

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto.

ATHARI ZITOKANAZO NA MAMA MJAMZITO KULALIA MGONGO | CHALI | TUMBO.
∆ Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama,
∆ Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono)
∆ Kushuka au kupanda kwa blood pressure
∆ Ini kuelemewa uzito
∆ Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto
∆ Kusikia kizunguzungu mara kwa mara
∆ Kama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku
∆ Kukoroma
∆ Maumivu ya mgongo
∆ Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen)
∆ Mtoto kukosa virutubisho vya kutosha.

MAMA ANASHAURIWA KULALIA MLALO GANI SALAMA
∆ Tafiti nyingi zinamshauri kwamba mama mjamzito alalie upande wa kushoto .Sababu damu husafirishwa kwa Urahisi zaidi kutoka kwenye moyo wa mama na kwenda kwenye kondo la mtoto na kumpa virutubisho vingi zaidi. .
∆ Iwapo mama atalalia tumbo au mgongo itamfanya mtoto asiwe comfortable atahangaika na kumpiga piga mama ili abadili position ya kulala.

USHAURI
∆ Mama anapolala ni vizuri akaweka mto katikati ya miguu usibane miguu ipitanishe, inakusaidia kulala comfortable,damu kusafirishwa vizuri na kutopata maumivu ya mgongo.Nyakati za usiku ni kawaida kwa watoto kupiga piga tumboni ,ila akipiga sana jua umelala vibaya anataka ubadilishe position.
                      
                        WELL - 0684127127 | 0743127127

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...