Skip to main content

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO
Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae.
Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama.
DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI.
• Kutokwa  na Damu ukeni
• Maumivu makali ya Tumbo
• Kuhisi kizungu zungu
• Maumivu makali ya kichwa
• Kutapika sana na kukosa hamu ya kula
• Kushindwa kuona
• Kupata degedege
• Kupata homa kali
• Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima
• Chupa kupasuka bila uchungu kuanza
• Kutoa mkojo kidogo
Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa.
• Uchunguzi wa kina
• Matibabu ya haraka
VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI.
• Kipimo cha Kaswende
• Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu
• Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo.
• Kipimo cha damu kuangalia group lako la damu Na mmeo
• Kipimo cha malaria
• Kipimo cha UKIMWI Kuangalia kama una maambukizi ili umkinge mtoto asipate maambukizi Wakati wa ujauzito, kujifungua na Wakati wa kunyonyesha.
• Kipimo cha haja kubwa kuangalia maambukizi ya minyoo
Mama ubainikapo unatatizo lolote hapo juu Jitahidi kuanza dawa ili kuepuka madhara na Magonjwa yapatikanayo kupitia Maradhi hayo.
Usiache kucomment hapo chini kwa maswali na ushauri.
Wasiliana nasi kwa Ushauri na Matibabu kwa Namba 0684/0743127127

Comments

  1. Mim ni mjamzito mimbq yangu inawiki 7 ila tangu jumanne naona damu kidogo nikienda choosing nikaenda hospital nikawaeleze wakanipima pia nikapiga ultrasound ikaonekana ipo vizuri na sasa bado naona damu kidogo nikienda chooni naombeni msaada weni

    ReplyDelete
  2. Mim mbna nahis kunavuta chini ya kitovu

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto. ATHARI ZITOKANAZO NA MAMA MJAMZITO KULALIA MGONGO | CHALI | TUMBO. ∆ Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama, ∆ Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono) ∆ Kushuka au kupanda kwa blood pressure ∆ Ini kuelemewa uzito ∆ Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto ∆ Kusikia kizunguzungu mara kwa mara ∆ Kama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku ∆ Kukoroma ∆ Maumivu ya mgongo ∆ Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen) ∆ Mtoto kukosa virutubi...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...