Skip to main content

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO AKIWA TUMBONI

Je wewe ni mjamzito na unatamani kufahama Hatua ya ukuaji wa mtoto wako aliyeko tumboni ??

Hizi ndio Hatua za ukuaji wa mwanao akiwa tumboni.

Hatua za ukuaji wa mtoto tumboni
WIKI YA (1- 4).
√  Yai la kike linarutubishwa na mbegu za kiume.
√  Kijusi kinaanza kujitengeza (Umba)
√  Mishipa ya damu,Tumbo,Ini, n.k vinatengenzwa

WIKI YA (5 - 8).
Viungo Muhimu vinatengenzwa na kukomaa

√  Ubongo
√  Moyo
√  Uti wa Mgongo
√  Macho,masikio,mdomo na pua.
√  Miguu, mikono, vidole na kucha

WIKI YA (9-12).

√  Shingo huanza kujitengenza.
√  Kope za macho hujitengeneza.
√  Katika kipindi hiki mtoto anafikia urefu wa inchi 2.5

Kumb.... Uhitaji mwingi wa madini ya chuma kwa mtoto.

WIKI YA (13-17).

√  Miguu na mikono inakamilika
√  Shingo inakamilika katika kipindi hiki.
√  Mifupa inaanza kukomaa

WIKI YA (18-22).

√  Mtoto anaweza  Kusikia sauti za mama yake.
√  Mtoto anaanza kucheza tumboni.
√  Mtoto anafikia urefu wa inchi 7.5 na uzito kuongezeka.
√  Unaweza Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto.

WIKI YA (23-27.

√  Vidole na kucha za mtoto zina kamilika.
√  Mtoto anaanza kulala na kuamka (kucheza)
√  Mtoto anaanza Kusikia sauti za nje na za mama.

Kumb.... Kuna uhitaji mkubwa sana katika kipindi hiki wa damu, Mama anaanza kuwa na upungufu wa damu kwa sababu uhitaji wa madini chuma kwa mama na mtoto ni mkubwa.

WIKI YA (28-32).

√  Ubongo wa mtoto unakamilika kutengenezwa na kukamilika.
√  Mtoto anaanza kufyonza virutubisho kwenye tumbo na utumbo mdogo wa mfumo wa mmeng’enyo wake.

WIKI YA (33-36).

√  Mboni za macho zinaweza kusinyaa na kutanuka, kuhisi mwanga.
√  Uzito unaongezeka maradufu zaidi kama ½ ya aliokuwa nao.
√  Kucheza na kuelea tumboni kunaongezeka zaidi na kwa nguvu zaidi.
√  Mifupa inakomaa na nywele zina kuwa zimeota.

WIKI YA (37-40).
√  Mtoto anakuwa tayari kwa kuzaliwa
√  Mtoto anaanza kushuka
√  Mama anaanza Kusikia chunguzi.
√  Maandalizi ya kujifungua

Kumb.... Uhitaji wa madini  ya chuma ni mkubwa sana kwa ukuaji na uborashaji wa afya ya mama na mtoto.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi wa namba 06841271271 | 0743127127
Usisahau kutoa maoni na mchango wako hapa chini ..

Comments

  1. Asante sana kwa ufafanuzi mzuri.

    ReplyDelete
  2. James Fuki kalunde - Ahasnte karibu tena kujifunza

    ReplyDelete
  3. Asante kwa ufafanuzi, Ila naomba kuuliza

    ReplyDelete
  4. Yeah nimejifunza na Nime enjoy good job!!!!!

    ReplyDelete
  5. Asante sana nimejifunza na kuelewa,, ili kuongeza madini ya chuma nahitaji kula vitu gani?

    ReplyDelete
  6. Asante sana nimefaidika vya kutosha

    ReplyDelete
  7. Nice I enjoyed the lesson I will do that thank

    ReplyDelete
  8. Asante sana kwa somo zuri, hakika limenijenga zaidi na nimejifunza mengi zaidi kupitia hili somo.

    ReplyDelete
  9. Asante kwa mafuzo lakin nataka unisadie nijue Kama mtoto na wakike au kiume

    ReplyDelete
  10. Asantee kwa SoMo zur nimejifunza kitu Niko second trimester ninahm ya kusikia but ulivofanya hapo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je tatizo la kutokwa na uchafu wa njano kipindi Cha ujauzito kuanzia miezi 8 ni Nini?

      Delete
  11. Je mtoto anakula vipi na anajisaidia vipi akiwa tumboni kwa mama yake?

    ReplyDelete
  12. Asante kwa somo zuri nimepata mengi yakufanya nilikiwa katika hatua hii

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto. ATHARI ZITOKANAZO NA MAMA MJAMZITO KULALIA MGONGO | CHALI | TUMBO. ∆ Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama, ∆ Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono) ∆ Kushuka au kupanda kwa blood pressure ∆ Ini kuelemewa uzito ∆ Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto ∆ Kusikia kizunguzungu mara kwa mara ∆ Kama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku ∆ Kukoroma ∆ Maumivu ya mgongo ∆ Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen) ∆ Mtoto kukosa virutubi...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...