Skip to main content

MAAMBUKIZI YA FANGASI KIPINDI CHA UJAUZITO | KIFAHAMU CHANZO | CHANZO | DALILI | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUJIKINGA.

MAAMBUKIZI YA FANGASI KIPINDI CHA UJAUZITO | KIFAHAMU CHANZO | CHANZO  | DALILI   | UCHUNGUZI  | MATIBABU | NAMNA YA KUJIKINGA.

FANGASI Ni maambukizi yanayoweza Jittokeza sehemu yoyote ya mwili.
Kuna aina kadha wa kadha ya fangasi na majina hutegemea na sehemu ya mwili walipo.

FANGASI WA UKENI - KIPINDI CHA UJAUZITO
Hawa ni moja ya fangasi ambao husumbua na hujitokeza kwa Wajawazito au kipindi cha Ujauzito na hushambulia sehemu ya uke.

Fangasi ambao hushambulia kipindi cha ujauzito wanajulikana kwa jina la candida albicans
Kipindi cha Ujauzito kuna mabdiliko ya Homoni ambazo kupelekea kubadilika kwa uasidi na ualikali (PH) ya Uke, na kuruhusu fangasi kuota kirahisi.

Kipindi cha ujauzito homoni aina ya estrojeni(estrogen) inakuwa nyingi kuliko zingine na kufanya mazingira rafiki kwa fangasi kuota.

Kuna sababu kadha wa kadha ambazo zinapelekea mjamzito kupata fangasi Mara kwa Mara .

CHANZO | SABABU
• Matumizi ya Dawa aina ya antibiotics Mara kwa Mara na kwa muda mrefu.
• Kuosha uke kwa maji na sabuni Mara kwa Mara (douching)
• Mabadiliko ya homoni kipindi cha ujauzito
• Matumizi ya vitu kama pafyumu au malashi, losheni kwenye uke.

DALILI
• Kuwasha ukeni
• Kutokwa na uchafu mweupe mzito kama maziwa mgando usio na harufu.
• Kuhisi Maumivu wakati wa kujamiana
• Kusikia maumivu kama vidonda wakati wa kujisaidia haja kubwa.

MADHARA YA FANGASI KWA MTOTO
• Mtoto kudumaa tumboni
• Mtoto kufia tumboni
• Matatizo ya kupumua
• Mtoto njiti
• Mtoto kuzaliwa na kilo ndogo
• Mtoto Wakati wa kuzaliwa anaweza kupata maambukizi ya fangasi na kuadhili Afya yake na ukuaji wake.

UCHUNGUZI NA MATIBABU NA NAMNA YA KUJIKINGA
• Mjamzito mewnye dalili kama hizi anashauriwa kufanyiwa vipimo vya maabara
• Mjamzito baada ya kuchunguzwa na kubainika anatatizo hilo anapewa dawa za kupachika ukeni.
• Epuka kuosha uke kwa maji na sabuni Mara kwa Mara.
• Safisha uke kwa kitambaa safi na kikavu.
• Tibu tatizo mapema kabla halijawa kubwa.
• Epuka Matumizi ya pafyumu, lotioni ukeni.
• Epuka Matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari.
• Tumia nguo za ndani aina ya pamba
•  Jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa.
• Epuka nguo za kubana.

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY MIMBA ZABIBU: Ni uvimbe unaotokea baada ya mbegu ya kiume kurutubisha yai la kike kwenye mji wa mimba (uzazi). Uvimbe huu baada ya kutengenezwa huendelea kukua na kuongezeka ukubwa kama mimba ya kawaida. Baada ya muda flani huanza kuleta au kuonyesha dalili za mtu Mwenye mimba au mjamzito. Uvimbe huu umetengenezwa na Tishu au kuta za mji wa mimba au uzazi. Kwa kawaida hali hii au uvimbe huu unaweza ukawa saratani au usiwe saratani, awali huanza kawaida ila kwa baadae unaweza ukawa saratani (kansa). NAMNA INAVYOTOKEA | CHANZO | KISABABISHI. Kwa kawaida ili mimba itungwe lazima mbegu ya kiume ikutane na yai la kike, na pande zote mbili upande wa mbegu za kiume na wakike lazima kuwe na vinasaba. Kama yai la kike halina vinasaba hutengeneza mimba zabibu (molar pregnancy) inayojulikana kama partial molar pregnancy, uvimbe huu huendelea kuongezeka ukubwa kama fung...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO AKIWA TUMBONI

Je wewe ni mjamzito na unatamani kufahama Hatua ya ukuaji wa mtoto wako aliyeko tumboni ?? Hizi ndio Hatua za ukuaji wa mwanao akiwa tumboni. Hatua za ukuaji wa mtoto tumboni WIKI YA (1- 4). √  Yai la kike linarutubishwa na mbegu za kiume. √  Kijusi kinaanza kujitengeza (Umba) √  Mishipa ya damu,Tumbo,Ini, n.k vinatengenzwa WIKI YA (5 - 8). Viungo Muhimu vinatengenzwa na kukomaa √  Ubongo √  Moyo √  Uti wa Mgongo √  Macho,masikio,mdomo na pua. √  Miguu, mikono, vidole na kucha WIKI YA (9-12). √  Shingo huanza kujitengenza. √  Kope za macho hujitengeneza. √  Katika kipindi hiki mtoto anafikia urefu wa inchi 2.5 Kumb .... Uhitaji mwingi wa madini ya chuma kwa mtoto. WIKI YA (13-17). √  Miguu na mikono inakamilika √  Shingo inakamilika katika kipindi hiki. √  Mifupa inaanza kukomaa WIKI YA (18-22). √  Mtoto anaweza  Kusikia sauti za mama yake. √  Mtoto anaanza kucheza tumboni. ...