Skip to main content

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KWA MWANAMKE

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI Ni moja ya sababu inayopelekea mwanamke Kushindwa kubeba /kushika mimba.

- Mirija ya Uzazi ina weza kuziba kwa sababu mbali mbali.
- Kuziba kwa mirija ya uzazi ni moja ya sababu kubwa ya Ugumba kwa wanawake.

SABABU ZINAZOWEZA PELEKEA MWANAMKE KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI NI...

- Kuwa na Uvimbe ambao umeota kwenye mirija ya uzaziz
- Kuwa na Ugonjwa wa maambukizi ya kizazi na Nyonga.
- Kuwa na historia ya mimba kutunga nje ya kizazi.
- Magonjwa ya zinaa na upasuaji wa tumbo au uvimbe kwenye ukuta wa uzazi.
- Kuwa na maambukizi kwenye mirija yaliyo sababishwa na utoaji wa mimba, kupasuka kwa kidole tumbo.
- Uzazi wa mpango (Lupu/Kitanzi)
- Ajari iliyo husisha Tumbo.
- Mirija kujaa maji.

DALILI ZA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI

- Maumivu wakati wa kujamiana /Tendo
- Maumivu makali ya nyonga na Tumbo kwa chini.
- Kupata hedhi matone ikiambatana na Maumivu makali/Kupata damu nyingi Wakati wa hedhi.
- Maumivu makali wakati wa kukojoa
- Maumivu makali ya Mugongo kwa chini/Kiuno
- Kuchoka sana

VIPIMO | MATIBABU | NAMNA YA KUZUIA /KUJIKINGA

- Vipimo vinapatikana kwenye vituo vya Afya Baada ya uchunguzi na Maelezo.
- Kipimo cha picha ya Tumbo
- Kipimo cha damu.
- Kipimo cha mkojo
- Matibabu hutolewa na mtoa Huduma wa Afya baada ya Maelezo na uchunguzi wa kina

NAMNA YA KUZUIA/KUJIKINGA
- Epuka utoaji mimba
- Tibu mapema magonjwa ya zinaa
- Chunguza/Pima Afya Mara kwa Mara.
- Wahi kituo cha Afya uonapo dalili kama hizi.
- Tumia Dozi kikamilifu

Kwa Maelezo na ushauri,Maswali andika hapa chini..

Kwa Maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba 0684127127-0743127127
WhatsApp :

Comments

Popular posts from this blog

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto. ATHARI ZITOKANAZO NA MAMA MJAMZITO KULALIA MGONGO | CHALI | TUMBO. ∆ Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama, ∆ Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono) ∆ Kushuka au kupanda kwa blood pressure ∆ Ini kuelemewa uzito ∆ Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto ∆ Kusikia kizunguzungu mara kwa mara ∆ Kama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku ∆ Kukoroma ∆ Maumivu ya mgongo ∆ Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen) ∆ Mtoto kukosa virutubi...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...