Skip to main content

MADHARA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI.

Kufanya mapenzi/kushiriki tendo wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana.

Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si mazuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi.

Yafatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati mwanamke yupo katika siku zake {period}

 MADHARA KWA MWANAUME.

1. Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.  

2. Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.  

3. Kuziba kwa njia ya mkojo.  

4. Utasa au ugumba.  

5. Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.  

6. Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida zisizo za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE.

1. Kupatwa na mambukizi viungo vya ndanivya uzazi  kama vile  shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.  

2. Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

3. Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.  

4. Utasa au Ugumba.  

5. Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.  

6. Athari mbaya ya kisaikolojia:
Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.
Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka hushiriki

Kwa mawasiliano zaidi 0684127127 | 0743127127

Kwa maoni na ushauri/maswali usisahau kutuandikia hapa chini.

Comments

Popular posts from this blog

IFAHAMU ARGI PLUS (+) MAANA YAKE | KAZI ZAKE | FAIDA ZAKE | MATUMIZI YAKE

IFAHAMU ARGI PLUS (+) MAANA YAKE | KAZI ZAKE | FAIDA ZAKE | MATUMIZI YAKE FOREVER Argi+ ni bidhaa bora kabisa kutoka katika kampuni yetu ya Forever living products Ina L-arginine amino acid kwa kila kijiko kimoja cha Argi+ Ina Nitric oxide ambayo inasaidia kutanua mishipa ya damu hivyo kuruhusu damu kupita vizuri Ina viondosha sumu vya *POMOGRANATE* ambavyo ni muhimu sana ili kuondoa sumu mwilini Ina *Vitamin* *Complex* ambazo zinasaidia kujenga misuli FAIDA ZA KUTUMIA ARGI+ 1. Ni kirutubisho muhimu sana kutumiwa kila siku kwa ajiili ya kusaidia mifumo yote ya mwili ili kuupa mwili uwezo wa kufanya kazi vizui zaidi. 2. Inasaidia mfumo wa kinga ya mwili, kutokana na nitric oxide ambayo inatumiwa na chembechembe nyeupe za damu kuua bacteria. Hivyo kuupa mwili uwezo zaidi wa kupigana na magonjwa. 3. Inasaidia kurekebisha kiwango cha "blood pressure kiwe sahihi na afya ya mzunguko wa damu ya moyo kiujumla. 4. Inasaidia kutengenezwa kwa mifupa na mwili kiujumla hivyo ...

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY

ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY MIMBA ZABIBU: Ni uvimbe unaotokea baada ya mbegu ya kiume kurutubisha yai la kike kwenye mji wa mimba (uzazi). Uvimbe huu baada ya kutengenezwa huendelea kukua na kuongezeka ukubwa kama mimba ya kawaida. Baada ya muda flani huanza kuleta au kuonyesha dalili za mtu Mwenye mimba au mjamzito. Uvimbe huu umetengenezwa na Tishu au kuta za mji wa mimba au uzazi. Kwa kawaida hali hii au uvimbe huu unaweza ukawa saratani au usiwe saratani, awali huanza kawaida ila kwa baadae unaweza ukawa saratani (kansa). NAMNA INAVYOTOKEA | CHANZO | KISABABISHI. Kwa kawaida ili mimba itungwe lazima mbegu ya kiume ikutane na yai la kike, na pande zote mbili upande wa mbegu za kiume na wakike lazima kuwe na vinasaba. Kama yai la kike halina vinasaba hutengeneza mimba zabibu (molar pregnancy) inayojulikana kama partial molar pregnancy, uvimbe huu huendelea kuongezeka ukubwa kama fung...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...