NJIA YA UZAZI WW MPANGO YA LUPU | KITANZI
LUPU (VITANZI) Ni moja ya njia ya uzazi wa mpango inayotumiwa na wanawake wengi kwa lengo la kuzuia kupata mimba au kupanga uzazi
Kifaa hiki kimetengenezwa kwa kutumia kopa kina kama vijitawi kwa mbele
Kifaa hiki kimetengenezwa na kuwekewa homoni ya Aina ya progestin ambayo inafanana sana na homoni aliyonayo mwanamke.
LUPU kina mkinga mwanamke asipate mimba kwa miaka 12.
JINSI GANI NJIA HII INAFANYA KAZI..
• Kina mkinga asipate mimba kwa muda wa miaka 12 kwa.
• Kutoruhusu mbegu za kiume kutofika kwenye mirija ya uzazi
• Huzuia urutubishaji wa yai la kike kama zikifanikiwa kuingia kwenye mji wa mimba
• Huzuia mbegu kuingia kwenye mji wa mimba kwenda kurutubisha yai la kike
FAIDA ZA NJIA HII..
• Inazui mimba zisizo na mpangilio
• Ni salama kwa mtumiaji
• Haisumbui kutoa na kuweka kwa mtumiaji
• Haichukui muda mrefu kurudi kwenye Hali ya kawaida na kupata mtoto. Wachache ndo huchelewa.
• Haisumbui kwatai wa tendo la ndoa
• Ni njia ya muda mrefu.
MAUDHI MADOGO MADOGO YA NJIA HII..
• Hedhi kubadilika
• Maumivu ya Tumbo
• Damu Kutoka wakati wa kiwekewa au kutotoka
• Kukosa hedhi
• Mwanamke hushauriwa kurudi kituo cha afya ka maudhi yataendelea kwa muda mrefu.
MTU YUPI ANASHAURIWA KUTUMIA NJIA HII.
• Anatumia mtu yeyote
• Awe ananyonyesha au ametoka kujifungua anaruhusiwa kutumia.
• Baada ya mimba kuharibika
• Awe ameolewa au hajaolewa
• Kazaa au bado kupata mtoto
• Mwenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi anatumia
• Mtu mwenye Shindikizo kubwa la damu.
WATU WACHACHE HUWEZA KUPATA SHIDA HIZI JAPO SIO WOTE BAADAYA KUTUMIA NJIA HII.
• Mji wa mimba kuvimba
• Mimba kutunga nje ya kizazi
• Kuchukua muda mrefu kupata ujauzito
Comments
Post a Comment