Skip to main content

KIFAHAMU KISUKARI KIPINDI CHA UJAUZITO | CHANZO/SABABU | DALILI ZAKE | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUKIEPUKA.

KIFAHAMU KISUKARI KIPINDI CHA UJAUZITO | CHANZO/SABABU | DALILI ZAKE | UCHUNGUZI | MATIBABU | NAMNA YA KUKIEPUKA.

KISUKARI Ni moja ya kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na  mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo

VITU VINAVYOWEZA KUPELEKEA MTU KUPATA KISUKARI:

♦ Kuwahi kujifungua mtoto mwenye Uzito mkubwa 4000g (4kg) kwa mimba/Ujauzito uliopita.
♦ Kuwa na historia kwenye familia ya mtu mwenye kisukari/kuridhi.
♦ Kuwa unene au Uzito mkubwa kuliko kawaida.
♦ Kuwa na shinikizo la juu la damu (presha)
♦ Kuwa na Mafuta mengi | cholesterol
♦ Kuwa na kisukari aina ya kwanza au ya pili.


AINA ZA KISUKARI:

Kuna ainaTatu za kisukari
KISUKARI AINA YA KWANZA | DIABETES TYPE 1
   
♦ Ni aina ya kisukari ambacho mtu anazaliwa nacho/kuridhi kutoka kwa familia yake.
♦ Hutokea tangu utotoni

KISUKARI AINA YA PILI | DIABETES TYPE (II)
  
♦ Ni aina ya kisukari ambacho mtu anakipata ukubwani
♦ Husabishwa na matatizo mbali mbali ya kiafya ambayo kwa uhalisia huzuilika mfano ulaji mbovu,matatizo ya moyo,Kutokufanya Mazoezi n.k

KISUKARI WAKATI WA UJAUZITO | GESTATIONAL DIABETES
   CHANZO

Mabadiliko ya Ulaji kipindi cha ujauzito.
     Mwanamke anapokuwa ameshika au kubeba ujauzito Ulaji unabadilika anakuwa anabagua baadhi ya vyakula.
     Kinacho sababisha aanze kubadili mlo ni hali ya kuwa na kichefuchefu na kutapika husababishwa na wingi wa homoni aina ya human chorionic gonadotropin (HCG)

Mabadiliko ya homoni (vichocheo)
     Kipindi hiki cha ujauzito kuna Mabadiliko ya mfumo wa homoni za mwanamke. Homoni zinazobadilika kipindi cha ujauzito ni estrogen na progesterone na human placental lactogen zina adhiri mmeng'enyo na ufanyaji kazi wa glukozi (glucose) pamoja na mafuta (fatty) kwenye damu 
      Homoni hizi hutengenezwa kwa kiasi kingi kisicho cha kawaida baada ya kutengenezwa kwa kondo la nyuma la uzazi (placenta)
      Baada ya homoni hizi kuzalishwa kwa wingi NA kuadhili glukozi na mafuta hupelekea kurundikana kwa punje punje za mafuta hayo na kudhibiti uchukuliwaji wa kiasi cha sukari kupelekwa kwenye seli kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kupelekea kubaki kwa kiasi kingi cha sukari kwenye damu.
      Kadri homoni hizi zinavyozidi kutolewa kwa wingi huenda kuadhili ufanyaji kazi/ufanisi halisi na utolewaji wa insulini kwenye kongosho kwa ajili ya kurekebisha kiasi cha sukari kwenye damu. Pia kupelekea matibabu ya kisukari kwa mjamzito kuwa magumu.
      Pia kupelekea kuadhili ufanisi bora/Kufanyaji kazi wa figo kupungua, na kuongezeka kwa kiasi cha damu yenye kiwango kingi cha sukari kwenye figo isinyo kawaida. Hali hii hupunguza ufyonzaji wa maji,damu,na vitu muhimu mwilini. Baada ya figo Kushindwa kufyonza maji yanayotakiwa kubaki mwilini kupelekea kiwango kingi cha maji kutolewa nje kwa njia ya mkojo, kipindi hiki mama huhisi na kujisikia haja ndogo Mara kwa Mara (kukojoa Mara kwa mara),kunywa maji mara kwa mara, kusikia kiu mara kwa mara.

DALILI ZA KISUKARI

♦ Kuhisi haja ndogo Mara kwa mara
♦ Kuhisi njaa Mara kwa mara na kula Mara kwa Mara.
♦ Kupungua Uzito kusiko kawaida
♦ Kusikia kia kiu ya kukaukiwa na maji Mara kwa Mara au kukauka mdomo Mara kwa Mara.
♦ Kushindwa kuona vizuri
♦ Kuchoka sana mara kwa mara
♦ Kusikia nganzi

UCHUNGUZI.

♦ Kipimo cha damu kabla ya kula chochote baada ya Massa sits kupita kuangalia kiwango cha sukari mwenye damu kwa wakati huo.
♦ Kipimo cha damu Muda wowote baada au kabla ya kula
♦ Kipimo cha damu masaa mawili (2) baada ya kula chakula kuangalia kiwango cha sukari mwenye damu.
♦ Kipimo cha mkojo kuangalia uwepo wa sukari mwenye mkojo wa mgonjwa.

MATIBABU.

Kila aina ya kisukari hutibiwa kwa dawa zake
♦ Kutumia dawa ulizoelekezwa kulingana na aina ya kisukari
♦ Kufanya Mazoezi ya mwili.
♦ Kuzingatia ulaji sahihi (mlo kamili)
♦ Kula Mboga mboga na matunda


MADHARA YATOKANAYO NA KISUKARI KWA MAMA

♦ Mama kupata matatizo ya miguu
♦ Mjamzito kupata uchungu/kuzaa kabla ya Muda.
♦ Matatizo ya macho
♦ Magonjwa ya mfumo ww mkojo ya mara kwa mara kama UTI, Fangasi wa ukeni.


MADHARA YATOKANAYO NA KISUKARI KWA MTOTO

♦ Mimba kutoka
♦ Mtoto kufia tumboni
♦ Mtoto kudumaa tumboni
♦ Mtoto kuzaliwa na kilo nyingi kuliko kawaida
♦ Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo
♦ Mtoto kuzaliwa na kisukari.

NAMNA YA KUEPUKA | KUZUIA KISUKARI.

♦ Zingatia ulaji sahihi (mlo kamili)
♦ Zingatia Mazoezi
♦ Zingatia Matumizi ya dawa kama ulivyoelekezwa
♦ Punguza uzito
♦ Epuka Mafuta yatengenezwayo kutoka kwa wanyama

Usisahau Kuandika maoni yako,maswali hapa chini.
Kwa mawasiliano zaidi tembelea mitandao yetu ya kijamii 

Instagram :https://www.instagram.com/lucyjohnbosco/
                  : https://www.instagram.com/wmclinic/
Facebook : https://www.facebook.com/welljambo/

Contacts  : 0684127127-0743127127 - https://wa.me/255684127127

Comments

Popular posts from this blog

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO

MAMA MJAMZITO ASILALIE TUMBO AU MGONGO Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto. ATHARI ZITOKANAZO NA MAMA MJAMZITO KULALIA MGONGO | CHALI | TUMBO. ∆ Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama, ∆ Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono) ∆ Kushuka au kupanda kwa blood pressure ∆ Ini kuelemewa uzito ∆ Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto ∆ Kusikia kizunguzungu mara kwa mara ∆ Kama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku ∆ Kukoroma ∆ Maumivu ya mgongo ∆ Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen) ∆ Mtoto kukosa virutubi...

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO Mama mjamzito yuko kwenye hatari ya kupata matatizo mengi yeye na mwanae. Matatizo hayo kujitokeza kwa ishara au dalili tofauti tofauti kulingana na aina ya tatizo alilonalo Mama. DALILI HIZI ZA HATARI KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kutokwa  na Damu ukeni • Maumivu makali ya Tumbo • Kuhisi kizungu zungu • Maumivu makali ya kichwa • Kutapika sana na kukosa hamu ya kula • Kushindwa kuona • Kupata degedege • Kupata homa kali • Mtoto kuacha kucheza | Kutokucheza siku nzima • Chupa kupasuka bila uchungu kuanza • Kutoa mkojo kidogo Mama mjamzito aonapo Dalili hizi anatakiwa kutoa taarifa haraka na kwenda kituo cha Afya kilicho karibu yake kwa. • Uchunguzi wa kina • Matibabu ya haraka VIPIMO VYA MUHIMU KIPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO NI . • Kipimo cha Kaswende • Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu • Kipimo cha mkojo kuangalia wingi wa protini na maambukizi ya njia ya mkojo. • Kipimo cha damu kuangalia gr...

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/ Ujauzito / mtoto   1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe 2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen      • Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A     • Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B     • Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB      • Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O 3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor  3.(a)     Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya + mfano A+, B+, AB+ au O+ 3. ...