VAGINAL DISCHARGE. (Kutokwa na uteute /Uchafu au majimaji kwenye uke) Miongoni mwa masomo ambayo tulijifunza huko nyuma ni juu ya umuhimu wa kutokwa na uteute au majimaji kwenye uke,somo liliwafungua wengi maana wengi walikuwa wakiona wanatokwa na ute bila kujua kazi yake au unaashiria nini. Mmbali na umuhimu wa uteute au majimaji yanayotoka kwenye uke, kumekuwa na maswali mengi na yanayoongozana kuhusu aina ya uteute unatoka kwenye uke, jambo ambalo limeonesha kuwapa hofu wengi juu ya afya zao pindi wauonapo ute ukiwatoka je kutokwa na uteute ni kawaida? Ndio,Tezi ndani ya uke wako na njia ya uzazi huzalisha kiasi kidogo cha majimaji ambacho hutuka kupitia uke kila siku, huku kikiwa kimebeba seli za zamani ambazo hazina kazi mwilini na kuzitoa kama uchafu, Hiyo ni njia ya kuufanya uke wake kuwa msafi na kulinda afya yake, ute huo unatoka huwa ni msafi wenye kuonekana vizuri au mfanano wa maziwa maziwa na hautoi harufu mbaya. (Uke kwa kawaida hautakiwi kuwa mkamvu, na tulishajifun...