ZIFAHAMU SABABU, DALILI, MATIBABU NA NAMNA YA KUZUIA TATIZO LA MIMBA ZABIBU | MOLAR PREGNANCY MIMBA ZABIBU: Ni uvimbe unaotokea baada ya mbegu ya kiume kurutubisha yai la kike kwenye mji wa mimba (uzazi). Uvimbe huu baada ya kutengenezwa huendelea kukua na kuongezeka ukubwa kama mimba ya kawaida. Baada ya muda flani huanza kuleta au kuonyesha dalili za mtu Mwenye mimba au mjamzito. Uvimbe huu umetengenezwa na Tishu au kuta za mji wa mimba au uzazi. Kwa kawaida hali hii au uvimbe huu unaweza ukawa saratani au usiwe saratani, awali huanza kawaida ila kwa baadae unaweza ukawa saratani (kansa). NAMNA INAVYOTOKEA | CHANZO | KISABABISHI. Kwa kawaida ili mimba itungwe lazima mbegu ya kiume ikutane na yai la kike, na pande zote mbili upande wa mbegu za kiume na wakike lazima kuwe na vinasaba. Kama yai la kike halina vinasaba hutengeneza mimba zabibu (molar pregnancy) inayojulikana kama partial molar pregnancy, uvimbe huu huendelea kuongezeka ukubwa kama fung...